Kabla ya kuingia katika Tasnia hii ya Filamu Tanzania, Mimi mwenyewe nilifanya Utafiti (Research) wa kina ili kujua ukweli na siri ya mafanikio ya Wasanii wale waliotoka kisanii na siri ya wale wasanii wasiotoka lakini wapo katika Tasia hii muda mrefu.
Katika utafiti huu nilipata majibu mawili makuu lakini kwa Asilimia tofauti. Kuna Suala la ushirikina, na Wizi wa kazi za wasanii wadogo. Haya ndio majibu ambayo yana tawala kuundermine our Arts in Tanzania.
Tukianza na Suala la ushirikina, wapo waliosema kuna kusafisha nyota nilishangaa sana kusikia watu wanaamini kuwa kunakitu kama hiki kwani kusafisha nyota, hakuwezi kufanikisha kumzuia masanii mmoja kutoka na mwingine asitoke katika sanaa, Wengine wanasema Kuzifanya kazi za sanaa za wenzao zisitoke huku wakiwatupia lawama wasanii waliotoka Hasa Tasnia ya Filamu kwamba zisitoke ili wao waendelee kutawala soko la Tanzania, wakisema mbona kazi zao silolote si chochote bali ni marudio ya kazi za zamani au wanacopy kazi wa Nigeria?
Wizi wa Kazi za Sanaa. Suala hili mimi naliamini kwa asilimia 80%, kwasababu ni suala sugu na limekuwa ni mchezo mdogo tu kwaWasanii wa Tanzania walio toka kisanaa, siyo Muziki, wala Sanaa hii ya Maigizo.
Kuna wizi wa aina nyingi.
Kunawizi wa Msanii kwa Msanii
Kuna wizi wa Distributor kwa msanii
Kuna wizi wa Kikundi cha sanaa kwa Msanii
aina hizi za wizi zinatokea hasa za Distributor kwa msanii, madistributor wengi nchini Tanzania si wakweli, ni wezi hawapendi kuiendeleza Tasnia hii ya filamu, Mukielewana kutoa Kopy 5000, basi ujue zitatoka 9000, bila Msanii kujua.
Lakini wizi huu hauwezi kuzuilika kama Kiwanda cha sanaa hakijatazamwa kwa jicho la Tatu kutoka Selikalini. Wasanii pia ni sawa na wafanya kazi wa Shirika au ofisi yeyote ile Tanzania au Selikalini. Wasanii wanahitaji Sheria kali ambayo itawalinda wao kupata haki wanayostahili kwa kiwango cha kueleweka.
OLawama nyingi nazipeleka kwa Wasanii ambao wanaibiwa kiolela Tanzaia, kunachombo kinaitwa COSOTA "Copyroght Society of Tanzania" Wengi hawasajiri kazi zao huku na ndio maana inakuwa kuzifuailia kazi zilizo ibiwa ambazo hazija sajiliwa ni ngumu sana. kwasababu wanashindwa kujua mmiliki halali wa lazi hiyo.
Wizi wa kazi za sanaa unaliathili soko na Tasnia ya filamu Tanzania kwani Wasanii wadogo wenye uwezo wanashindwa kuonesha vipaji vyao kwani kazi zao zinaibiwa na Wasanii wakubwa.