Dec 28, 2017

MTUMISHI WA MUNGU SILVANUS MUMBA AACHIA NURU

Muimbajiwa Nyimbo za Injili Tanzania ametoa Albam yake ya kwanza iitwayo NURU, Akiongea na Blog hii Silvanus Mumba ambaye pia ni Muubiri na Muinjilist amesema Album yake ina nyimbo 8 ambazi Mungu alimuonesa na kumtaka aimbe ili watu wapatekupokea uponyaji wa kiroho na kimwili

Mumba alisema Watu wainunue Album yake wasikie kilicopo kwani anasema Nyimbo yake ya kwanza iitwayo NITASUBIRI ilifanya vizuri sana na kumfanya ajisikie Faraja  kwa Mapokezi mazuri, ambayo Watanzania na Washabiki wa mziki wa Injili Duniani waliupokea na kuusifu kuwa ni wimbo Bora



Ziko nyimbo nyingi Kali na Nzuri sana kwa kuzisikia, kuburudika, na kujifunza, munapokea uponyaji kupitia Wimbo mmojammoja ulioimbwa katika Album yangu anasema Silvanus

Kuusikia Wimbo wa Kwanza uitwao Nitasubiri check hapa,

NITASUBIRI - SILVANUS MUMBA

Kuipata AlbumhiiMpigie moja kwa moja Mtumisi wa MunguSilvanus Mumba kupitia
Simu: 0713073280

Wasiliana naye kupitia
Facebook @revmumba
Instagram @silvanusmumba
Twitter      @silvanusmumba

Jun 27, 2017

TAMASHA LA DADA JACKLINE SKAMWA, KUFANYIKA JUMAPILI HII 2/07/2017

Akiongea na Mwandishi wetu, Jackline Skamwa anasena, anawashukuru sana Ndugu Silvanus Mumba (Muinjilist na Muimbaji wa Kimataifa) pia John Mgina (Kichaa wa Yesu) na Merciana Mwakapasa, Kwa kuwa naye Bega kwa bega katika maandalizi ya Uzinduzi wa Imefunguka (Mchum Yesu)

Waimbaji watakao hudumu ni wengi mno na Tamasha hilo, litakuwa la Kipekee sana, Anasema hategemei kuchangisha kitu chochote, isipokuwa atakaye Guswa na Albam yake au kupenda kuendeleza huduma hiyo, basi atamsupport kwa kununua Albam yake, ili aweze kufanya tamasha kubwa zaidi la kumtukuza Mungu.

Muimbaji Silvanus Mumba pia atakuwepo na waimbaji wa kwenye picha ifuatayo hapa chini, wote watahudumu









HAKUNA KIINGILIO, NI BUREEEEEE, NJOONI TUMSIFU MUNGU






Tamasha hili litafanyikia katika kanisa la OASIS HEALING MINISTRY (OHM) Ka Mchungaji NTEPA. KANISA  hili lipo nyuma ya Ubungo Plaza, ukifika hapo ulizia Kwa mchungaji ntepa utakuwa umefika. 
au Piga simu number 0713073280

Jun 14, 2017

BAADHI YA WAIMBAJI KWENYE TAMASHA LA BIG PRAISE CONCERT, SILVANUS MUMBA YUMO

Gazet lako la mtandaoni la Peruzi Gospel limekutana na Waandaaji wa BIG PRAISE Concert ambalo litafanyika Jumapili hii tarehe 18June 2017 Pale FPCT kurasini. Tamasha hili limekuwa Gumzo kubwa Nje na Ndani ya Nchi kwa jinsi maandalizi yake yalivyo pamba moto na kuchukua hisia za watu mbali mbali wa kubwa kiasi kwamba hata viongozi wa kisiasa kuliongelea kuwa ni Tamasha litakalo tikisa jiji na Tanzania kwa ujumla.

Wametaja list kubwa sana ya waimbaji lakini Muimbaji wa kimataifa SILVANUS MUMBA, EMMANUEL MBASHA, BISHOP ABRAH, BEATRICE KITAULI, BAHATI SIMWICHE NI BAADHI YAO, KUPATA LIST MAMILI ANGALIA PICHA HAPA CHINI WOTE WATAKUWEPO KATIKA KUFANYA KAZI INAKAMILIKA













HAKIKA TUTAUONA UWEPO WA BWANA TAMASHA HILI SIO LAKUKOSA KABISA, MAANA MAPRODUCER, MADIRECTOR NA WADAU WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA WATAKUTANA NA WAIMBAJI NA WAHUBIRI INJILI KATIKA STAGE MOJA. KIINGILIO NI BURE KABISA

MUMBAJI WA INJILI TANZANIA SILVANUS MUMBA AGEUKA KUWA DILI

Muimbaji wa Nyimbo za Injli Tanzania ajulikanaye kwa jina la Silvanus Mumba, aka Reverent Silvanus Mumba, amekuwa Deal au Talk of the Town nchini Zambia, Congo, Malawi na South Africa, Baada ya Tamasha lake alilo lifanya Hivi Karibuni Ndola nchini Zambia.

Akiongea na Muandishi wetu hapa Zambia, alisema anapendwa kwa nyimbo zake ambazo zimewekwa vionjo vya kizazi kipya na yeye anabarikiwa sana na uimbaji wake binafsi, lakini pia kupitia huduma yake ya uimbaji wengi wamepata kuokolewa na wengine kupata uponyaji. 

Silanus amsema Albam yake ipo tayari na soon itakuwa released, anacho subiri ni Uongozi wake umruhusu tu aanze mchakato ili watu wapate kuburudishwa na vibao vilivyopo katika Albam hiyo. 

Mimbaji huyo ambaye anamuonekano mzuri (HB) amesema anapata usumbufu mkubwa sana especial kwa wasichana wanaojigonga kwakwe ili wamteke kimapenzi, lakini yeye anamsimamo mmoja tu, anafanya sanaa ya uimbaji kwaajiri ya Kumtukuza Mungu hivyo mambo mengine hawezi kuyachanganya katika kazi yake.  

Aidha Silvanus amesema kwa sasa yuko chimbo kuandaa Albam yake ya pili yenye vibao vikali hatari, ambavyo ataanza kuviachia mwezi December mwaka huu, huku akiwaomba washabiki wake wa nchi za jirani wakae mkao wa kula. alipo ulizwa kwanini Tanzania hakubaliki sana alijibu kuwa Nabii awiki nyumbani ingawa na nchini Tanzania anamatamasha makubwa mawili ambayo amesema lazima atafanya mabalaa makubwa sana ili watu wajifunze kupitia yeye. 

Matamasha hayo ni BIG PRAISE CONCERT  na TAMASHA LA SIFA AMBAYO imembidi asimamishe shughuli zake zote kwaajiri ya kujiandaa na Matamasha hayo, Muimbaji huyo amesema waandaaji wengi wa Matamasha wanamuogopa kutokana na status yake na Elimu yake, lakini amewatoa hofu kuwa Kwenye uimbaji status ya maisha inakaa pembeni na Gharama za kumchukua si kubwa kama wanavyo fikiria,

Silvanus Mumba anapatikama kwa Contacts:  
WHATSAPP:   0713073280
FACEBOOK:     Silvanus C. Mumba 
INSTAGRAM: silvanusmumba


Peruzzi na Mimi.