Jun 25, 2011

Zombi kama inamkosi vile

Ile filamu   ambayo niliriport juzi kuwa imefikia katika hatua za mwisho za finalization, imeingia mkosi ambao tokea niota kichwa changu haujawahi kutokea machoni mwangu. Movie hiyo katika Siku hii yaleo juma pili tarehe 25 june 2011 nimetamani kulia na kucheka kwa wakati mmoja lakini na kujionea huruma mimi na pia Editor wangu.

It was like the movie file didn't open for almost three hours we were trying to open it... finally we failed and start again newly the first scene editing.. i said this because i know wadau wataniona kama si muaminifu kwa kuwapa mzuka wa filamu hiyo..

kwa maana hiyo basi filamu hiyo itachelewa kidogo kutokana na insidence hiyo..Nawaomba radhi wote walio kuwa na big expectations about this filamu

Jun 24, 2011

Filamu ya Zombi Bado kidogo Kuisha Editing

Ile filamu ambayo niliiongelea mwezi mmoja ulio pita kwamba nataka kuiandaa ije kufundisha nini kinafanyika katika matendo ya giza ipo karibu kumalizika maandalizi ya Awali. Filamu hiyo ambayo ime andaliwa na ndugu Silvanus C. Mumba (executive produser) na kuchezwa na wasanii mahili sana akiwemo Shiva, Nyemo mabalwe, na wasanii chipukizi wengi wakiwa katika hali ya kimataifa,

Editing ya filamu hiyo imefanyika Hapa Dar es salaam na Mtaalamu kutoka nchini ufaransa kwa jina Awax, na ni professional wa kufanya filamu za aina hiyo, Director wa filamu hiyo ni ndugu Silvanus Mumba ambaye alicheza kama Main character akisaidiana na Awax ambaye alikuwa Camera man.

Naomba ndugu wadau wa filamu mukae mkao wa kula kuisubiria Filamu hiyo iliyo sheheni mafundisho ya kutosha na intertainments, refreshments, comedy, na mengineyo

Jun 13, 2011

SILVANUS C. MUMBA: Nimepata Idea ya kuwasajili wasanii Wote Tanzania

SILVANUS C. MUMBA: Nimepata Idea ya kuwasajili wasanii Wote Tanzania: "Siku moja nilikuwa natokea viwanja vya Leaders, Nikakutana na Mtu akiwa na Idea mzuri sana ya kuwasajili Wasanii, Lakini nilipo jaribu kumuh..."

Nimepata Idea ya kuwasajili wasanii Wote Tanzania

Siku moja nilikuwa natokea viwanja vya Leaders, Nikakutana na Mtu akiwa na Idea mzuri sana ya kuwasajili Wasanii, Lakini nilipo jaribu kumuhoji vizuri alikuwa yupo kipesa tu na si kwa nia mzuri,
Sitaki kusema idea yake ni mbaya La hasha bali nia yake iliyo nyuma ya usajili huo ndiyo mbaya.

Ninacho taka kusema ni kwamba hiyo idea ni nzuri sana katika Kipindi hiki ambacho wasanii hutafuta njia ya kutokea, hasa wasanii wadogo. Nilijisikia vibaya sana kuona umati wa takribani watu 2000, wakisubiri interview ya kuchukuliwa kucheza filam ya Ruge Mutahaba kutoka Clouds FM. kulikuwa na Mtitu pamoja na wakina Zamaradi Mketema.

Kilicho niuma zaidi ni kuona vijana wali walivyo na uwezo mkubwa wa kuvaa uhusika katika tasnia hiyo ya filamu, lakini mwisho wa siku walichukuliwa watu kumi tu. hii inanifanya nirudi nyuma na kuanza kujipanga upya kutafuta njia ya kuwawezesha vijana hawa waweze kujikwamua kimaisha.

Vijana wengi wasanii ambao bado hawajatoka, wamekuana na mikingamo mingisana ikiwemo Kutapeliwa pesa zao na vinginevyo. Yaani anaweza tokea mtu na kujifanya yeye ni executive produser, anaanza kuwachangisha Pesa wasanii kisha kuwadanganya wataandaa filamu ya Pamoja na wasanii, cha kushangaza anatokomea gizani bila majibu na kuwaacha wasanii hao solemba, nashukuru Mungu huwa hawakati Tamaa lakini nasema: SELIKALI IKO WAPI? AU WANAJISIKIA VIZURI SANA WANANCHI WAO WANAVYO TESEKA HIVI WAKATI NJIA ZA KUWASAIDIA ZIPO?

Mimi nasema kama wao hawazioni waje kwangu kuniuliza nitawapa njia,, kwangu moto ni < Ora et Labora> sara na kazi (mtakatifu Benedicto)

Jun 1, 2011

Filamu ya Zombie Peak ya Holywood

Nyemo Mabalwe
Huyu ni NYEMORITHA MABALWE
Katika Filamu hii ya ZOMBI amefanya makamuzi ya kufa mtu, na alikutana na magumu mengi sana lakini aliyashinda Challangez hizo ni pamoja na Kuumia, na alisimama yeye kama make up Designer wa Wasanii akishirikiana na KAKA YAKE SILVANUS MUMBA, ambao kwa ujumla ndiyo ma main characters wa filamu hiyo.  Nyemo amecheza kama RITHA Mke wa Russo (SILVANUS) ambaye ni kaka yake wa Damu kabisa lakini kwenye Movie hii ya kutisha na kusisimua waliweka ukaka na udana Pembeni na kufanya makamuzi ya kufa mtu.

Huyu ni Silvanus Mumba
KAKA WA NYEMO. Kijana Silvanus amesimama kama ZOMBI make up designer na ambecheza kama main character katika filamu hiyo ya kusisimua. Silvanus anasema kwa makamuzi aliyo yafanya katika filamu hiyo hana budi kuwaambia Watanzania wote wakae makao wa kula Kusubiri msisimko na Uhondo ulioko katika filamu hiyo ya Kizombie.
Silvanus amejigamba kuwa hata stori yake imetulia na aliitunga kwa kufuata directives za kimataifa na si kukurupuka katika utunzi wa story na Script. Silvanus ameidirect yeye mwenyewe kwasababu amesema Tanzania hakuna Director ambaye angeweza kuidirect filamu hiyo kwasababu wengi wao hukurupuka kufanya kazi ambazo hawana nature nayo wala background ya kazi na mwisho wa siku wanaishia kuiharibu kazi.

Naomba ndigi watanzania muisubiri kwa hamu FILAMU hiyo itakayo kuja kwa jina la ZOMBI.
Raymond Mtapulo
Kijana Ray amecheza Kama Jose Rafiki yake RUSSO, Raymond amecheza kama rafiki wa karibu sana na Russo na ni best friend wa Familia ya Russo, Makazi aliyo yafanya kwenye filamu hii si ya kusimulika lakini mimi nawasihi Watanzania kuisubiri kwa hamu kubwa sana Movie hii.
Charles Magali anasema Yeye amefanya makamuzi ambayo hajawahi kuyafanya katika Movies zote alizocheza Hapa Tanzania kwahiyo Watanzania wakae mkao wa kula kuisubiria Movie hiyo.
Akiongea na Blog hii, Mzee Magali amesema Huyu Director wa Movie hii anauwezo wa Kimataifa na atafika Mbali kwani amemtabiria kufikia peak ya Hollywood.