Jun 13, 2011

Nimepata Idea ya kuwasajili wasanii Wote Tanzania

Siku moja nilikuwa natokea viwanja vya Leaders, Nikakutana na Mtu akiwa na Idea mzuri sana ya kuwasajili Wasanii, Lakini nilipo jaribu kumuhoji vizuri alikuwa yupo kipesa tu na si kwa nia mzuri,
Sitaki kusema idea yake ni mbaya La hasha bali nia yake iliyo nyuma ya usajili huo ndiyo mbaya.

Ninacho taka kusema ni kwamba hiyo idea ni nzuri sana katika Kipindi hiki ambacho wasanii hutafuta njia ya kutokea, hasa wasanii wadogo. Nilijisikia vibaya sana kuona umati wa takribani watu 2000, wakisubiri interview ya kuchukuliwa kucheza filam ya Ruge Mutahaba kutoka Clouds FM. kulikuwa na Mtitu pamoja na wakina Zamaradi Mketema.

Kilicho niuma zaidi ni kuona vijana wali walivyo na uwezo mkubwa wa kuvaa uhusika katika tasnia hiyo ya filamu, lakini mwisho wa siku walichukuliwa watu kumi tu. hii inanifanya nirudi nyuma na kuanza kujipanga upya kutafuta njia ya kuwawezesha vijana hawa waweze kujikwamua kimaisha.

Vijana wengi wasanii ambao bado hawajatoka, wamekuana na mikingamo mingisana ikiwemo Kutapeliwa pesa zao na vinginevyo. Yaani anaweza tokea mtu na kujifanya yeye ni executive produser, anaanza kuwachangisha Pesa wasanii kisha kuwadanganya wataandaa filamu ya Pamoja na wasanii, cha kushangaza anatokomea gizani bila majibu na kuwaacha wasanii hao solemba, nashukuru Mungu huwa hawakati Tamaa lakini nasema: SELIKALI IKO WAPI? AU WANAJISIKIA VIZURI SANA WANANCHI WAO WANAVYO TESEKA HIVI WAKATI NJIA ZA KUWASAIDIA ZIPO?

Mimi nasema kama wao hawazioni waje kwangu kuniuliza nitawapa njia,, kwangu moto ni < Ora et Labora> sara na kazi (mtakatifu Benedicto)