Mar 21, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UTEUZI NA UHAMISHO WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UTEUZI
NA UHAMISHO WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo, Jumatano, Machi 21, 2012 ameteua Makatibu Tawala wa Mikoa saba na kufanya uhamisho wa wengine watatu.Ifuatayo chini ni taarifa kamili iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue ikitangaza uteuzi huo:-

A: MAKATIBU TAWALA WA MIKOA
1.       Dkt. Faisal Hassan Haji ISSA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa KILIMANJARO. Kabla ya hapo Dkt. Faisal alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
2.       Bibi Mariam Amri MTUNGUJA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MBEYA. Kabla ya hapo Bibi Mtunguja alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.
3.       Bwana Eliya Mtinangi NTANDU, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MOROGORO. Kabla ya hapo Bwana Ntandu alikuwaKatibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Dar es Salaam.
4.       Bwana Severine Bimbona Marco KAHITWA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Bwana Kahitwa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dodoma.
5.       Eng. Emmanuel N.M. KALOBELO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa KATAVI. Kabla ya hapo Eng. Kalobelo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasharui ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
6.       Bwana Hassan Mpapi BENDEYEKO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa RUVUMA. Kabla ya hapo Bwana Bendeyeko alikuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.
7.       Dkt. Anselem Herbert Shauri TARIMO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa SHINYANGA. Kabla ya hapo Dkt. Tarimo alikuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.Uteuzi huu unaanzia tarehe 21 Machi, 2012. Wataapishwa Ikulu, Jumamosi tarehe 24 Machi, 2012 saa nne asubuhi.

: UHAMISHO
1.       Bibi Mgeni BARUANI – Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro anahamishiwa Mkoa wa NJOMBE.
2.       Bibi Mwamvua A. JILUMBI – Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga anahamishiwa Mkoa wa SIMIYU.
3.       Bibi Bertha O. SWAI, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya anahamishiwa Mkoa wa PWANI.
4.       Balozi Ombeni Y. Sefue

KATIBU MKUU KIONGOZI
IKULU,
DAR ES SALAM.
21 Machi, 2012


Silvanus

No comments: