Aug 2, 2011

Msanii ni nani?

Msani ni kiyoo cha jamii,
Msanii ni mtu anaye jiheshimu na kujitunza
Msanii anajua utu wake anatunza heshima ya wenzake na kutunza heshima ya utamaduniwake
Msanii ni Mshauri wa jamii,
Msanii ni Mbunifu, mgunduzi na Mtafiti wa mambo yenye tija katika jamii
Msanii ni mtu asiye penda kashfa, na ni mpenda maendeleo,
Msanii ni mfano wa jamii, kwa Tabia njema na kupenda kukosoa vitu ambavyo havina tija kwa jamii
Msanii ni kiongozi wa jamii
Msanii ni nguzo ya jamii katika uelimishaji, na uanzishaji wa mambo mbalimbali ya kimaendeleo.
Msanii ni Mburudishaji jamii
Msanii ni mfanya kazi za kijamii, nani mfano wa kuigwa katika jamii husika

Huyu si msanii
Mwenye Kashfa nyingi
Mwenye kupenda kufanya vitu vya kushangaza jamii
Mkaa uchi
Mpenda umbea
Asiye na aiba ya ushauri wala ubunifu wenye tija
Asiye na Mapenzi mema na Wahusika wa utamaduni wake

Makosa ya Wasanii wetu
Kwanza hupenda sana sifa zisizo na tija kwao na kwenye jamii
Hawapendi kujielemisha na kusoma zaidi
Hawana kisomo, na wanakashfa nyingi sana za mapenzi na utembeaji wa uchi,
Kuonyesha vitendo vya ndani nje ya jamii inayo wazunguka
Hawana akili ya kuiwakilisha jamii katika sehemu yeyote ile
Si mfano wa kuigwa katika jamii, kwasababu ukiwaiga utapotea

Tufanye nini?
Tuunde chombo ambacho kitawawajibisha wasanii hao,
Tuunde chombo ambacho kita wasuport katika Kazi zao
Tuunde chombo ambacho kitakuwa kinasimamia Nidhamu na kazi zao
Kuunda chombo ambacho kitakuwa na uwezo wa kuwakumbusha Elimu ni ufunguo wa maisha
Kuunda chombo kitakacho wafuatilia wasanii hao na kuwapongea wanapofanya vizuri
Chombo hicho kiwe na nguvu ya kuwafungia wasanii wenye Nidhamu mbovu