May 23, 2012

Kifilamu Tumepiga Hatua, Lakini Turekebishe Hivi kwanza

  1. Wasanii walioshiba husika. wasanii wenye uwezo wa kuvaa uhusika wa mahali husika, Mfano Kijijini "Kama ni washamba basi waoneshe ushamba wa pekee, na si kuvaa nguo chafu kama wafanyavyo wasanii wengine, unaweza kuwa msafi lakini kuna usafi wa kijijini ambao ukija mjini unaonekana kabisa wewe ni wa kijijini, Uongeaji na utembeaji, nywele, na hata pozi zako, zinatakiwa zifanane na uanakijiji.
  2. Story inayofanana na mazingira uliyopo. Maranyingi wasanii wetu wanasahau kuwa Mazingira ya kitanzania yana visa vyake ambavyo ukivicheza hivyo unaweza kutumia nguvu kidogo sana kuvaa uhusika kuliko visa vya kuiga kutoka Filamu za wenzetu. Mfano unaweza cheza Visa vya Kishirikina na kuhusu kuua Wazee wenye macho mekundu, au Albino, au Wizi wa Vibaka wadogowadogo, au Story wa Makabila mbalimbali, usaliti, uchawi, uvunjaji sheria nakadhalika
  3. Location zisiwe bandia.. unakuta mtu kamaliza Chuo hapohapo anakuwa na pesa na Jumba kubwa na magari ya kifahari. Nataka kuongelea Location kwasababu uhalisia wa kuishi maisha ya kifahari kwa Tanzania ni mdogo sana, na tukifanya Sensa leo hii tutatambua kuwa karibu asilimia 80% ya Watanzania hawaishi maisha hayo, kwahiyo Location zetu zifanane na ujumbe unaotaka kuufikisha, na tusipende kuwaonesha Watanzania kuwa Maisha ni rahisi hivyo kuyapatia. Mfano wa Location zinazo fanana na Utanzania ni Nyumba ya kawaida na isiyo na geti kama ni Mzuri lakini isiwe ya kifahari, Ofisi ya kawaida, Selikali za mitaa na si Polisi za Bandia, Mitaa iliyo ya kiswahilini na si kimjini, kwasababu asilimia 90% ya watanzania wanaishi uswahilini.
  4. Script writers. Hawa watu hupenda kuandika vitu ambavyo havipo katika uhalisia wa Kitanzania. Jaman napenda kuwakumbusha kuwa Matumizi ya Lugha za kigeni Si unogeshaji wa Filamu, Ukitumia Lugha ya Kitamaduni utanogesha zaidi na kupromote Nchi yako na kabila lako. inashauriwa kutumia Lugha zinazofanana na Hata unapo andika Script angalia mazigira ya Scene na maongezi yanayo ongelewa na uhalisia Wa kitanzania. Mfano Watu wanatongozana ofisini, Ki uhalisia Watanzania ni watu wenye Aibu sana, na hata kama anamtamani sana mtu huyo ataomba kukutana naye sehemu nyingine, na hata kama ni mpenzi wake hawezi kuanza kumshikashika ofisini ambapo watu wengi huingia na kutoka kufuata huduma ya mwenyeofisi,.. Lakini Waandishi wanapenda kuandika vitu kamahivi.
  5. Directors. Hawa ndio waaribifu wa Filamu zetu kwa Asilimia Kubwa sana. Bila kujua story Director huwezi kudirect Movie, lakini Madirector wa Bongo wanadirect Scene kwa Scene bila kujua Story inataka nini, mwisho wa siku unakuta mwisho kuna Baadhi ya Scene zinakataana. na hii inatokana na uvivu wa Madirectors kusoma Story. Kingine ni kulazimisha vitu visivyo na msingi Mfano Mtu akikimbia kuonesha amekimbia vizuri basi aanguke, au Kama kunadimbwi la maji akanyage. au Kama Jambazi Basi Avae makoti makubwa machafu au Mawani tinted au makofia, au kutembea na Silaha za moto hazarani, au kukunjakunja uso na kadhalika. Kumbe vitu hivi tumekuwa tukijidanganya na ndomaana Filamu zetu zinakosa uhalisia.
  6. Mavazi. kunamsanii Mmoja ni Mama lakini sitataja Jina lake. Amerudia gauni moja kwenye Filamu zaid ya Tatu. sasa unakuta filamu hii kavaa, ingine tena kavaa na nyingine tena, na Produsers wanampa pesa na Madirectors wanaona hawawezi kosoa kwasababu ni Wazembe wa Kufanya Research. Mavazi yanajenga Heshima mtaani na hata kwenye kazi ya Sanaa. Wengine huvaa Nusu uchi Hasa hawa DADA ZETU. inakera na haimaanishi Kuwa mchezaji bora ni kuvaa uchi, mbona Wasanii wa kiume hawavai vingua vya ajabu, na wanapata umaarufu na ni masupastaa tu?
  7. Action Wasanii wa kibongo wanadhani kuongea sana ndo kuigiza Vizuri. kumbe Expression ndo usanii, uhusika unavaa vipi, unaguswa vipi na tukio fulani. sasa unakuta mtu ili aonekane amekasirika anaanza kubwabwaja maneno kwa nguvu na sauti kubwa, na kadhalika, Wasanii wa Kibongo ni waongo sana kwenye kushtuka, Kushangaa, na hata kukimbia kwa hamaki.
Ushauri
Producer
  1. Andaa budgeti ya kutosha, kwaajiri ya kuwalipa wasanii na kufacilitate shughuli mzima
  2. Fanya  Research ya kutosha kuwapata wasanii wazuri kwaajiri ya kutengeneza kitu kilicho Bora.
  3. Andaa Kambi au basi Sehemu ya kufanyia Mazoezi walau wasanii wajue Scene watakazocheza zinahitaji nini, na kuwaweka sawa pale kwenye makisa
  4. Chagua Director Mzuri
  5. Chagua Story mzuri na Story mzuri ni ile yenye mwanzo mzuri Kati panapo eleweka na Mwisho wenye muendelezo au wenyemaana.
  6. Andaa Kila kitu kwa ushirikiano wa Director
  7. Chagua Wapigapicha na Camera nzuri
Director
  1. Soma story kabla hujakubali kazi
  2. Shiriki kwenye Mazoezi utoe ushauri wako
  3. Kagua wasanii kama wameiva kuicheza story hiyo
  4. Kagua Locations na usipende sifa bila kujituma
  5. Toa Maelekezo na si lawama kwa msanii
Msanii
  1. Kuwa mbunifu wa kucheza na kuvaa uhusika
  2. Cheza kushirikisha mwili mzima na usipanick
  3. Sikiliza maelekezo kutoka kwa Director
  4. Kama kunakitu kinakutatanisha uliza na kama ni kinyume na Maadili usikubali kucheza
  5. Andaa Nguo za heshima na si za aibu
Madistributor
ACHENI USHAMBA WA MASTAA
Kunafilamu nyingi na mzuri zinazo vutia hazina mastaa, inawasanii mahili na wamecheza vizuri sana kuliko hata hao mastar, lakini huwa munaziacha hii kasumba ni mbovu na siipendi kabisa.

Cameraman

Naomba niishie Hapo maana ninamengi ya kuzungumza lakini Muda haunitoshi Asanteni sana nakaribisha Maoni, na yatajibiwa Bila shaka.

No comments: