Jun 5, 2012

Huu ndo ujinga wa Gwantwa (Anti Ezekiel)

Alikula pesa ya watu kiasi cha shilingi Milioni 1. kutoka kampuni ya AF production, Kwa makubaliano ya kutengeneza filamu ambayo watu mpaka sasa wako Location wanashoot,
Cha kushangaza kufikia siku ya juma mosi taree 2. ambayo walikubaliana kukutana ili waanze kambi ya Shooting hiyo hakutokea, na simu akazima, Sasa kitimbi kilikuja siku ya jumapili wakati akipigiwa simu bila kupokea. Mkurugenzi wa kampuni ya AF Production akaamua kutumia simu ya msanii mwingine ili kuangalia je anafanya makusudi.
Baada ya kupiga haikuita sana akapokea, na kuulizwa je unakuja kambini hauji? Jibu alilo toa nikuwa kesho yake angesafiri kuelekea Dubai kunakazi anakwenda kufanya. kulikuwa na mvutano wa maneno na Mkurugenzi huyo anayefahamika kwa jina la MWAJUMA SAID MOHAMED akaamua kuomba ushauri, kwanza akamuomba kakayake aitwae SILVANUS MUMBA, na kukubaliana kitu.
Kufikia Saasita usiku mkurugenzi akifuatana na team yake walitimba mpaka kituo cha polisi Oysterbay na kuriport tatizo hilo na Ant akapigiwa simu hapo hapo, Bila kuchelewa akafika kuogopa Amri ya polisi.
Mazungumzo yaliendelea na Anti akakubali kulipa kiasi hicho na pesa za usumbufu, tukaachana na mimi nikaenda kulala.

Ila wasanii munajidhalilisha jamani, hii si hali mzuri na yule ni huruma tu ya Mkurugenzi tulitaka kumualibia Safari yake kwasababu yeye kaaribu kazi ya watu.

No comments: