Mar 31, 2011

Handsome sasa Kuitwa Salome..

Kutokana na Maoni ya Wadau mbalimbali ambao tunashirikiana nao katika kuandaa Filamu zetu ili ziwe Bora zaidi, wameshauri Jina la Handsome lisitumike katika filamu hiyo Bali badala yake litumike jina la SALOME...

Kwamujibu wa Executive Produser Ndugu Silvanus C. Mumba (Coordimator, KOICA) amesema Management yake imelidhia jina hilo na sasa Filamu hiyo inayotarajia kuingia Sokoni mapema Mwezi wa NNE imesheheni Vitimbi mbalimbali vya kiuswahilini, Mafindisho ya kijamii, Kisiasa, kiuchumi na hata kitechnolojia.

Katibu wa Kundi la SAFARI Arts Group ndugu Raymond Mtapulo (Mavitu) Amesema kwasasa wao wanakazi moja tu ya kutoa Mawe ya nguvu (akimaanisha Filamu zenye ubora wa juu kuliko hata filamu zilizowahi kutoka Tanzania)

Mama Mlezi naye aliongezea akisema Wasanii wake wananidhamu ya kimchezo kutokana na hilo hana wasiwasi na Wasanii hao ambao kwa pamoja wamecheza kwa kiwango cha kimataifa na Hata Editing imeeditiwa na EDITOR kutoka Nchini CONGO ambaye alikuwa anafanya kazizake nchini UFARANSA.

Watu wakae mkao wa kula ili wapate kile moyo unapenda na Wizara naSelikali ijiandae kupata faida na Utambulisho mpya Kimataifa kwa filamu hiyo..

No comments: