Jan 28, 2013

MWANAMAPINDUZI

MWANAMAPINDUZI

Movement yeyote ya Kufanya mapinduzi, hasa mapinduzi makubwa kwa selikali iwe ya kijeshi au ya kimaendeleo, ni lazima mtu Mmoja aumie ili wafaidike wengi.

Wanafalsafa wengi sana kutoka ulimwenguni, huubariki msemo huu na hata vitabu vya Mungu vinautakasa kwani (kwa wakristo Yesu alikufa Msalabani kwaajili ya Dhambi za wengi duniani) na kwa waislamu pia Mitume wengi walipoteza Maisha yao kwaajili ya Haki za wanaimani wenzie na ndiyomaana leo hii tunakula Matunda yake.

Ninacho taka kusema ni kipi, Wana Tunduru, huu si muda wa kulaumiana wala kumlaumu yule, huu ni wakati wa kukaa chini na kuulizana Tulikosea wapi na tuparekebishe kwa njia Gani, Mimi binafsi nikisikia wapo watu wenye uwezo wa kufanya Mapinduzi ya Kielimu na Kimaendeleo, ambayo ndiyo kikwazo kikubwa cha wana Tunduru wengi kunyanyasika.

Movement itaanzia kwenye TUDURU DEVELOPMENT FORUM, ambayo inamjengwa wa kuwaunganisha wanatunduru wote, Wenye mapenzi mema na Tunduru yao, na Wenye uchu wa Maendeleo, na Wenyekutaka wanaTunduru leo hii wakomboke kutoka kwenye Utumwa huru, na kuwa Watu wenye kufanya Mbinu na itifaki za kimaendeleo wao Wenyewe.

Elimu yetu ipo chini sana,
Wazazi wa Wana Tunduru naomba muniunge mkono kwa kuwapeleka watoto wenu shule, Tafadhali elimu ya shule ya msingi kwa sasa haina thamani hat kidogo, na wala Elimu ya Kidato cha nne kadhalia, Staili ya sasa ni kumpeleka Mwanao Chuo akapata elimu Kombozi, kwani kutokea hapo ataweza kupata ajira.

Watoto wa kike
Msiharakie kuwa na familia (kuzaa mapema si utajiri Bali ni kujiandalia umasikini) Nasema hivyo kwani kuna wengi sana Wana harakia kuzaa wakati hawana vyanzo vya kiuchumi, hata akitokea mtu akitaka kukusaidia kielimu anakuta kuna kikwazo cha mtoto, anashindwa kuendelea.. Akikupeleka wewe shule Nani atamlea mtoto wako?

Vijana Tunduru'
Kila kukicha Ajira za kujiajiri zina zaliwa sana tu (TUTAKUJA NA TUDEFO kuhamasisha hata vikoba ili watu waweze kutengeneza hcannels za kuweka na kukopa wao wenyewe kwa wenyewe, kwani Tunduru (ukitaka kuendelea jenga ushrika) Mabiashara makubwa yote unayoyaona si ya mtu mmoja bali na watu wengi wakafanya wazo la Pamoja na kufanya mkataba wa ushirikiano (Article of association) na Memorandum of Understanding kwaajiri ya kuendeleza Kipato chao,

Natoa rai kwa Wana tunduru wote, Tushirikiane kurekebisha Mawazo hayo kisha tujenge msingi imara wa kimaendeleo (tukiopna kiongozi ana tuangusha katika jitihada zetu, 2015 tusimchague hiyo ni msaliti wetu,)

nawasilisha

Peruzzi na Mimi.

No comments: