MTU mmoja ambaye hajafahamika jina amekuwa na tabia ya kutapeli watu kwa kutumia simu ambapo amekuwa akijifanya ni mtu unayemfahamu na huomba msaada wa fedha.
Mtu huyo ambaye anatumia namba 0714 530 869 na 0716 494 259 amekuwa akijitambulisha kwa jina la mtu unayemfahamu sana na hutoa taarifa kuwa simu yake ina matatizo kidogo hivyo kukuomba umtumie kiasi fulani cha fedha kwa kuwa ana matatizo na yupo mkutanoni.
Aidha, tapeli huyo hataki kabisa uongee naye bila shaka kwa kujua kuwa utamtambua na badala yake hukuomba uwasiliane naye kwa njia ya sms.
Mara nyingine atakuambia kuwa ana mgonjwa na mtumie fedha kwa namba ya mjomba wake. Atakupa ahadi pia kuwa ukimtumia hizo fedha, atazirejesha. UKITUMA TU, UMEUMIA. Chukueni tahadhari. Katika ofisi za mtandao huu ametuma sms kwa wafanyakazi wengi lakini ameambulia patupu! Namba moja (inayoishia 259) ameisajili Tigo Pesa kwa jina la LWITIKO MWANJOKA lakini nyingine hajaisajili. Wizi anaoutumia ni wa kijinga sana, lakini naamini kati ya watu 20, angalau 2 huwapata! Mjulishe na mwenzio, usitume fedha kwa mtu usiyemjua, hata akitumia jina la mzazi wako!
Peruzzi na Mimi.
No comments:
Post a Comment