Ushauri kwa Wasanii wa Filamu (Wanafilamu)
Tanzania
Kutokana na kutokea kwa kifo cha Msanii nguli wa Filamu Tanzania Juma Kilowoko almahalufu SAJUKI,
Nina machache sana ya kuzungumza na Wasanii,
Wadau na Waandaaji wa filamu Tanzania.
Sajuki ni msanii ambaye alikuwa na nia ya
kufika mbali na kazi zake zote alizo cheza zilikuwa na mafundisho makubwa mno.
Sajuki alikuwa na Mapenzi ya kweli nay a dhati kwa mkewe na wasanii wengine.
Mimi namchukulia Sajuki kama mpiganaji, Muelimishaji na mcheshi. Namuombea
Baraka tele Wastara kwa kuondokewa na kipenzi chake Sajuki.
Lakini katika mambo ninayo taka kuongea ni
hili la kuzingatia sana Bima ya Afya (Medical Insurance), na Mifuko ya kijamii
kwa Wasanii.
Jambo hili ni lamsingi sana kwa wasanii
kulitolea Macho. Mimi nashangaa sana Eti kuna Raisi wa Shirikisho la filami
Tanzania ambaye hana hata Baraza la Mawaziri wala Kamati Tendaji yenye kuleta
Tija katika Tasnia hii ya Filamu Tanzania.
Ningewaona Wenye Busara sana kama kungekuwa na
Mipango mikakati ya kila Mwaka katika kuhakikisha kuwa Wasanii ambao wako chini
ya Raisi wao SIMON MWAKIFAMBA. wanapata vitu vile vya msingi ikiwemo na Medical
Insurance, pamoja na kuhakikisha wanajiunga na mifuko ya kijamii, kama NSSF, LAPF,
PSPF, na mingine mingi, ili kujiwekea akiba ya uzeeni au hata litokeapo janga
au ugonjwa Kama ulio mkuta Ndugu yetu Sajuki.
Sitakikusema nilikuwa nashubiri litokee jambo
au nichukulie msiba wa SAJUKI kama mfano lakini nachukulia kama Fundisho la
Kila msanii na Huyo RAISI WA SHIRIKISHO ajaribu kufikiria mbinu za kuwanasua
kwenye umasikini wa kimawazo Wasanii anao waongoza.
Wenzetu wana Medical Insurance na nilazima kwa
msanii yeyote anayecheza Filamu ama Tamthilia kujiunga na BIMA YA AFYA, iko
kwenye sheria ya nchi na hiyo walipropose wenyewe wasanii. Hiyo Moja, mbili
Lazima msanii aweanalipa kodi ya kila kazi yake inapo ingia sokoni ili kulinda
sells flow na mwisho apate kilicho hakiyake, kwa uhakiki wa mamlaka za mapato.
Mwisho napenda kuwapa pole Wasanii wote,
nikiwepo na mimi, kwa msiba mkubwa sana kuondokewa na nduguyetu Sajuki
Mpiganaji, ila Tuungane tupiganie haki zetu na Tukumbuke Afya zetu.
Mungu ailaze Roho ya marehemu Pema peponi
amen.
With Regards
Silvanus
C. Mumba
Volunteers
Program Coordinator
0713073280/ 0752014077
KOICA
Tanzania Office
Phone:
022 244 2324
Fax:
022 244 2297
Peruzzi na Mimi.
No comments:
Post a Comment