Nov 30, 2012

SENIOR GEOLOGIST WITH DIAMOND AND KIMBERLITE EXPERIENCE

SENIOR GEOLOGIST WITH DIAMOND AND KIMBERLITE EXPERIENCE

My client requires an experienced geologist to come on board for a 6 month contract in Lesotho beginning in January. The ideal geologist should have at least ten years’ experience exploring in remote environments for diamonds and kimberlites.
I also have a full time position available in Angola. The skills required are very similar although it is a permanent position. If you feel any of these opportunities are of interest please do not hesitate to get in touch.
james@pangea-resourcing.com


Peruzzi na Mimi.

Nov 26, 2012

R.I.P Sharo-Milionea




Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constatine Masawe amekiri kutokea kwa msiba wa Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’, baada ya kupata ajali katika kijiji cha Lusanga, Muheza akiwa katika gari lenye namba za usajili T478 BVR Toyota Harrier, majira ya saa mbili usiku, ambapo pia ndio nyumbani kwao.

Sasa naweza kusema R.I.P Sharomilonea. Maiti ya Sharo Milionea imehifadhiwa hospitali ya Teule Muheza.

Kuhusu Habari ya Mazishi tutataarifiana tupatapo updates kutoka kwa Ndugu wa karibu

PERUZZI NA MIMI IPO PAMOJA NA NYI MLIOGUSWA NA MATATIZO HAYA, NA KUMUOMBEA KWA MUNGU AMPOKEE.. BWANA ALITOA NA BWANA ALITWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE SASA NA HATA MILELE AMEN.


Peruzzi na Mimi.

Nov 18, 2012

AY AMEIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA CHANEL O

  AY ndio msanii pekee kutoka TANZANIA (East Africa) aliyenyakuwa tuzo ya Channel O Music Video Award kwa mwaka huu 2012 katika kipengele cha MOST GIFTED AFRICAN EAST VIDEO OF THE YEAR. Video iliyochukuwa tuzo hiyo ni I DON'T WANT TO BE ALONE akiwa amewashirikisha wasanii kutoka Nairobi Kenya wanakwenda kwa jina la Sauti Sol.
 Msanini AY naweza Mfananisha na Muigizaji Wa Tanzania Marehemu Steven Kanumba ambaye aliamua kutoboa anga za kimataifa na kufanya filamu na Wanaigeria ikiwa ni njia yake ya kutafuta kipato lakini akiitangaza nchi yetu ya Tanzania,  Kanumba kwasababu yeye anathubutu kutonoa Border  na kwenda nje ya Tanzania na hata nje ya Africa kufanya muziki tofauti na wasanii wenye majina hapa Bongo kwetu.
Tunapaswa kuiga mfano mzuri wa Ndugu yetu msanii AY, ili tuweze ipeperusha Bendela ya Tanzania kwa nchi mataifa mengine. hii itatusaidia hata katika utalii wtu wa Ndani na wa nje kwani tutawavutia wengi kuja kutalii na kuiongezea Nchi fedha za kigeni.
Peruzzi na Mimi.

Nov 13, 2012

RIP Mariam Khamis wa TOT

Msanii wa taarab nchini Tanzania wa kundi la TOT plus, Mariam Khamis maarufu kama paka mapepe amefariki dunia usiku wa jana kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam mara tu baada ya kujifungua .

Mariam Khamis umauti umemkumba akiwa anaimba kundi la TOT plus lakini enzi za uhai wake aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya taarab likiwemo East Africa Melody, Zanzibar Stars na 5 Stars.

Khamis Muhidini Shomary baba wa marehemu amesema mipango ya mazishi inaendelea kufanyika ambapo anatarajiwa kuzikwa hapo kesho Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.


Mariam akiwa kwenye Poz


Silvanus

Nov 9, 2012

Mrembo wangu wa Ijumaa hii

Naanza kwa kumpongeza mrembo na mwanamitindo Karrueche Tran kwa uwamuzi wake wa Busara aliouchukua wa kuachana boyfriend wake,Chris Brown.

Hivi karibuni vyombo vingi vya habari vimeripoti kuhusu mrembo na mwana mitindoKarrueche Tran kuachana na mwimbaji / maarufu ambae anapenda sana kuwanyanyasa girlfriend zake pale anapokuwa nao.

Taarifa zilizoenea katika mitandao hivi karibuni zinadai mwimbaji huyo amerudiana na girlfriend wake wa zamani"RiRi" nadhani mpaka hapo umesha jua namzungumzia nani,huyu si mwingine ni dude,Chris Brown.

Na kama wewe unaamini na kukubali alicho sema Chris,kuwa amemuacha Karrueche, kwa sababu hakutaka kuona Karrueche anaumizwa na uhusiano wake na ex-girlfriend wake Rihanna.

Na hivi karibuni Chris amepost video mtandaoni ili mashabiki wake ulimwengu kote wajue,“Hey, y’all, Rihanna’s really hot and famous. So I’m gonna break up with my model girlfriend and try and hook up with Rihanna again.

Baada ya hayo yote je unamjua Karrueche Tran ni nani, ni mwanamke tu ambae alitaka kuwa na Brown? Huyu ni mwanamitindo toka Vietnamese ambae anaishi nchini marekani na ambae ana miliki matandao unaohusika na vyakula na huku aki hangs out na watu maarufu kama, er, Chris Brown na binti wa Rev Run’s ambae ni Angela Simmons.

Kiukweli Karrueche Tran ni Mrembo na nina mkubali angalia tu baadhi ya picha zake we mwenyewe utakubali.

LEAH atafanya vitu vya Ajabu Soom

JINA la Lamata si ngeni sana kwa wadau wa filamu hapa nchini, Lamata jina lake halisi ni Leah Richard Mwendamseke katika makala ya leo anapata nafasi ya kuongelea fani yake katika tasnia ya filamu Swahihiliwood, Lamata lizaliwa Jijini Mbeya alipata elimu yake ya Shule ya msingi katika shule ya Ukuti darasa la kwanza hadi la tano.

Baadae alihamishiwa shule ya msingi Karobe na kusoma darasa la sita na kumalizia la saba, shule ya Sekondari alisoma Arage kidato cha kwanza na pili huko Mbeya kuhamishiwa katika shule ya sekondari ya Wanging’ombe Mkoani Iringa kidatu cha tano na sita Perfect vision.
Sanaa ya uigizaji alianza rasmi mwaka 2008 katika kikundi cha sanaa cha Amka ambao walikuwa wanarusha michezo yao kituo cha televisheni cha ITV, Lamata akiwa katika kundi hilo aliaanza kama muigizaji na ailiigiza sehemu chache katika mchezo wa Ndoano, baadae aliaanza kuandika script.

“Mnamo mwaka 2009 nikaanza kufanya kazi katika kampuni ya RJ chini ya uongozi wa director VIncent Kigosi ( Ray) kama Production manager,kwa kushirikiana na kampuni hiyo nikaanza kujifunza kazi ya udirector,kuna madirector wengi walionisaidia kama Vicent Kigosi,Selles Mapunda na Adam Kuambiana, pamona msaada kutoka kwa waongozaji tofauti tofauti Ray ndio alinipa msaada mkubwa,”anasema Lamata.



Mwanadada huyo anasema kuwa katika kufunzwa huko hakuishia kupokea mafunzo hayo tu lakini hiyo haikutosha alianza kujifunza zaidi kupitia mitandao mbalimbali inayohusiana na filamu na vile vile kusoma vitabu mbali mbali, Kazi hiyo ilimsaidia kupata urahisi kwa kuwa alikuwa ni mpenzi wa kuangalia filamu tangu utoto wake, tabaia ambayo ameendelea nayo hadi sasa ya kupenda sana kuangalia filamu hasa za nje ili kujifunza zaidi kwa kuona wenzetu wanafanya nini na sisi tuko wapi.