Nov 9, 2012

LEAH atafanya vitu vya Ajabu Soom

JINA la Lamata si ngeni sana kwa wadau wa filamu hapa nchini, Lamata jina lake halisi ni Leah Richard Mwendamseke katika makala ya leo anapata nafasi ya kuongelea fani yake katika tasnia ya filamu Swahihiliwood, Lamata lizaliwa Jijini Mbeya alipata elimu yake ya Shule ya msingi katika shule ya Ukuti darasa la kwanza hadi la tano.

Baadae alihamishiwa shule ya msingi Karobe na kusoma darasa la sita na kumalizia la saba, shule ya Sekondari alisoma Arage kidato cha kwanza na pili huko Mbeya kuhamishiwa katika shule ya sekondari ya Wanging’ombe Mkoani Iringa kidatu cha tano na sita Perfect vision.
Sanaa ya uigizaji alianza rasmi mwaka 2008 katika kikundi cha sanaa cha Amka ambao walikuwa wanarusha michezo yao kituo cha televisheni cha ITV, Lamata akiwa katika kundi hilo aliaanza kama muigizaji na ailiigiza sehemu chache katika mchezo wa Ndoano, baadae aliaanza kuandika script.

“Mnamo mwaka 2009 nikaanza kufanya kazi katika kampuni ya RJ chini ya uongozi wa director VIncent Kigosi ( Ray) kama Production manager,kwa kushirikiana na kampuni hiyo nikaanza kujifunza kazi ya udirector,kuna madirector wengi walionisaidia kama Vicent Kigosi,Selles Mapunda na Adam Kuambiana, pamona msaada kutoka kwa waongozaji tofauti tofauti Ray ndio alinipa msaada mkubwa,”anasema Lamata.



Mwanadada huyo anasema kuwa katika kufunzwa huko hakuishia kupokea mafunzo hayo tu lakini hiyo haikutosha alianza kujifunza zaidi kupitia mitandao mbalimbali inayohusiana na filamu na vile vile kusoma vitabu mbali mbali, Kazi hiyo ilimsaidia kupata urahisi kwa kuwa alikuwa ni mpenzi wa kuangalia filamu tangu utoto wake, tabaia ambayo ameendelea nayo hadi sasa ya kupenda sana kuangalia filamu hasa za nje ili kujifunza zaidi kwa kuona wenzetu wanafanya nini na sisi tuko wapi.

1 comment:

papa mutombo said...

Nakupa hongera sn na unaweza mama endelea hivo hivo by redisony23@gmail.com