Apr 19, 2012

FreeMason

Historia ya Freemason imegawanyika katika Nyakati kuu mbili tofauti, Yaani Kabla na baada ya Grand Lodge of England on 24th June 1717. Baada ya kutengenezwa kwa Grand Lodge huko Uingereza ambazo zilikuwa maalumu kwa Freemason, Freemason walianza kuenea Duniani kote kwa kutengeneza Lodges za mtindo huohuo katika nchi nyingine, na sasa ikafika hadi Tanzania, Kabla ya ukoloni. Marekani ilifika Mwaka 1775.

Ningependa kuwapa kazi ambazo wao huwa wanazifanya na Tabia za watu hawa ambao wapo kwenye Dini hiyo ya Kishetani.

1. Kusaidia watu wote wenye matatizo mbali mbali, Mfano majanga kama kwetu hapa Gongolamboto, Mbagalia Mabomu, Mafuliko, Kuunguliwa Moto nakadhalika 

2. Kusaidia vituo vya watoto yatima, Kuandaa sikukuu au mikutano ya vilema na wamama wajane.

3. Wanatoa misaada ya kupata kazi na awakati mwingine facilities na njia mbadala za kupata kazi.

Tabia zao 

1. Kwanza ni wapole na wanyenyekevu sana kwa watu na hawapendi makundi yenye kujitoa kimbelembele.

2. Wengi wao ni matajiri na watu maarufu, na wenye Heshima kubwa sana kwenye nchi husika, na wafanyabiashara.

3. Watu wanaopenda kujitolea kwa hali na mali katika jamii, ikitokea tatizo lolote la kitaifa.

4. Wanaopenda kuanzisha mifuko mbalimbali kwaajili ya jamii Fulani, Lengo ni kupata

5. Hawapendi ugomvi au machafuko ya aina yoyote, ni watu wa Amani.

6. Hutumia Ufreemason wao kupata wateja kwenye biashara zao, au kupata watu wengi kwenye majukwaa ya kisiasa kwa lengo la kushinda chaguzi mbalimbali, kwa wanamuziki Ili miziki yao ipendwe na kupata watu wengi kwenye shoo zao. Wachezaji kwa Fowadi waweze kushinda magoli wawapo kwenye mechi, na Waigizaji kazizao zipendwe na wao wawe na followers wengi.


Alama zao

Hizi ni alama wanazo tumia Mara kwa mara wakiwa kwenye shugulizao kwaajiri ya kuleta mvuto kutoka kwa watu wanao wasikiliza au wanaofuata Burudani kwa Wanamuziki Kama Michael Jackson. 

Pia kwa Wachezaji wanaishara ya Vidole Viwili kuonesha chini (cha pili na cha tatu kutoka dole gumba) wakati wa kupiga faulo, na Penalt. au wakikaribia Goli wakati wa Kufunga ( Messi, Ronaldo ) ni mifano mzuri.


Freemason in Tanzania

Mpaka sasa Dini hii ya kishetani inamiaka zaidi ya 79, toka ilipoingia hapa nchini Tanzania na member wake wamezidi kuongezeka na kuwa wengine sana kati ya miaka ya 1985- 2000 kwa kutaka kupata Mvuto kisiasa, Kiutamaduni, Kimichezo, Kimuziki, Uigizaji na wengine katika biashara na mambo mengine. Lakini hili la Siasa ndo limeshika hatamu sana, Tafadhali Fuatilia Mikutano ya Bunge na uone Je Ishara hizo hapo juu hazitumiki? Jibu unalo wewe!!!




Hili ni Hall lililoko Mtaa wa sokoine Liko mkabala na Hotel ya Kilimanjaro Kempisky, na wageni wengi hufikia Hotel hiyo kwa urahisi wa Mikutano yao, kwani mambo yao huendeshwa kwa usiri mkubwa sana.


Hawa ni Mafreemason Wakishiriki kwa Pamoja katika shughuli ya upandaji wa Miti, Nadhani sasa utaanza kuelewa Kazi na shughuli wanazo jishughulisha na hawa watu,, NAOMBA TUWE MAKINI SANA NA HAWA WATU, AMBAO HUFANYA VITU VINGI VIZURI ILI KUKUVUTA NA WEWE UJIUNGE. FUMBA MACHO MKUMBUKE MUNGU WAKO KISHA WAKEMEE.





Huyu Jamaa ANAITWA Sir Andy Chande Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Yeye ni Mwanachama wa Freemasons

Hawa jamaa hapa Tanzania wamesaidia kituo cha watu wenye ukoma cha kindiwi wilayani Utete; Kituo cha watoto cha Mama Theresa; shule  ya Vipofu ya Pongwe, mkoani Tanga; Kituo cha yatima cha Arusha, Hospitali ya Mnazi mmoja kula Zanzibar; na Shule ya Viziwi ya Buguruni.







Hiyo ni Form Maalumu ya kujiunga na Hao watu na ukisha jiunga situation inakuwa kama hivyo hapo kwenye picha.

Wanahitaji nini

1. Kujua siri ambazo Mungu amezificha kuhusu Binadamu, na Umungu, na kuisambaza dini yao Duniani kote kwa kupaza sauti yao, ili sikumoja Shetani atawale Dunia

2. Wanataka Dunianzima waabudu Mfumo wa Sayari (Pentagram Cycle of Venus. )ambao wao ndo Mungu wao

3. Kudesign and kujenga miji Muhimu na mikubwa duniani kama Washington

4. Na kuiteka Dunia ili wawe na wafuasi Wengi kuliko wanao Muabudu Mungu

Ushauri Wangu.

Jamani Hawawatu wanatumia njia nyingi sana kuwarubuni watu Duniani Kote, Na mara nyingine hutuma Messages kwa Hardcoppy au Emails kudanganya kuwa Wao walifanikiwa kwa kusambaza ujumbe huo kwa watu wengi (huwa inakuwa kuanzia 7 hadi 14)

Hawamuabudu Mungu na wanamuabudu shetani, na Dini yao inanguvu sana imewateka Watu wazito wote unaowajua wewe Tanzania, Kenya Uganda na Duniani kote, Kama unavyoona Picha hapo juu


Freemason wanaabudu hiki hapo juu.

Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600 wa kundi la watu wenye imani ya siri ya Freemasons wakiwa wanatokana na watu wa kada mbalimbali wakiwemo maarufu, huku ikielezwa kwamba miongoni mwao hakuna viongozi wakuu wa serikali.

Hayo yalibainishwa na Kiongozi wa kundi la Freemasons katika eneo la Afrika Mashariki, Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Sir Andy Chande alipozungumza na gazeti hili (HabariLeo), wiki hii Dar es Salaam.

Kiongozi huyo Mtanzania mkazi wa Dar es Salaam mwenye asili ya Kiasia, alisema licha ya Tanzania kuwa na wanachama hao, kwa sasa idadi ya wanachama duniani inapungua tofauti na inavyoonekana sasa kuwa wanaongezeka kutokana na kuibuka maneno mengi kuhusu kundi hilo.

Alisisitiza kuwa si rahisi kumjua mwanachama wa kundi hilo, bali wenyewe ndio wanaofahamiana, akisema ni siri na kwamba wenyewe wanakutana katika vikao mbalimbali mara moja kwa mwezi au zaidi.

Alisema nchini kuna wanachama wakiwemo wafanyabiashara, watumishi serikalini, walimu pamoja na wanataaluma mbalimbali wanaoheshimika sana na kusisitiza kuwa kuna maneno mengi yanayosemwa kuhusu kundi hilo, ambayo siyo ya kweli. Alisema idadi ya wanachama wake duniani inazidi kupungua kutoka milioni nane hadi sasa wako milioni sita, tofauti na wengi wanaodhani kuwa idadi hiyo inaongezeka.

Chande alizungumza na mwandishi wa habari hizi katika Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert ambako yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule alipozungumzia maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, alisema duniani kuna watu wazito wengi ambao ni wanachama wa kundi hilo kama majaji wakubwa na hata Binamu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza ni kiongozi mkubwa wa kundi hilo.

Akizungumzia masharti ya kujiunga na kundi hilo, Chande alisema ni lazima mwanachama huyo awe anaamini katika Mungu bila kubagua iwapo ni Mkristo au Muislamu.

Alisema pia ni lazima anayetaka kujiunga awe na umri unaozidi miaka 21 na walio chini ya umri huo hawaruhusiwi kujiunga na lazima familia ya anayetaka kujiunga na wanandugu wafahamu kuwa umejiunga na kundi hilo.

“Unajua katika imani hii kuna michango mbalimbali ambayo unatakiwa kutoa ambayo ni zaidi ya dola milioni sita (karibu Sh bilioni 10), hivyo ni lazima ndugu wafahamu ili kuepuka matatizo utakapotakiwa kutoa,” alisisitiza.

Alisema si kweli kuwa wenye fedha wengi ni wanachama wa kundi hilo huku akikanusha wanachama wanajiunga kwa ajili ya kupata fedha, bali ni dini kama imani nyingine. Alisisitiza kuwa hakuna ukweli kwamba wanaopata mafanikio katika maisha wakiwa ndani ya imani ya Freemasons kuwa wanatoa kafara watu wao wa karibu kwa lengo la kupata utajiri.

Chande pia alisema hairuhusiwi kutumia jina la kundi hilo kwa nia ya kujipatia nafasi sehemu mbalimbali au kuongeza nafasi katika chuo au shule.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/09/freemasons-wanachama-kujiunga-muhtasari-wa-aliyoyasema-sir-andy-chande.html#ixzz2PYL6Jw00

Nadhani sasa nimejibu maswali mengi ya watu na kama kuna kingine kunahitaji kujua basi tuulizane tu kwa kutumia Address Hiyo hapo chini. 


(Mimi si member wa Freemason Tafadhali Naomba nieleweke Hivyo)


Silvanus C. Mumba
Dar es Salaam

Silvanus

1 comment:

Mustapha MaDish said...

Angalau nimepata kujuajua kuhusu hawa jamaa maana naona kila mtu anasema lake so thanx jombaa!!