May 17, 2019

SILVANUS MUMBA: PANGA MALENGO YAKO KWA KUTUMIA SMART OBJECTIVES



Silvanus mumba Vijana wengi na wafanya biashara wengi, wale wa Biashara ndogondogo na zile biashara kubwa, hawapendi kupanga malengo yao, na ndio maana biashara zao zinakuwa sio za uhakika. utaenda mwaka huu utamkuta akiuza samaki, mwakani anauza karanga, kwasababu hawana mipango na hawajui jins ya kuifanya iwe mipango endelevu.

Peruzzi na Mimi.

Apr 12, 2019

SILVANUS MUMBA: USIPOKUWA MUAMINIFU HUWEZI KUPATA WASHIRIKA KIBIASHARA


Silvanus Mumba ni Professional Human Resources Manager with since 2009 working as Administrator (KOICA) Program Coordinator (KOICA) HR Officer (Vipajilink) HR Manager (CRSG) HR Manager (Sunshine Mining) and HR Consultant (Hadithi Zetu Limited)

Silvanus Mumba is a Gospel artist and Motivational speaker too, doing his Motiations jobs through Video Podcasts on his YouTube channel, Here is his one of the Motivation Videos.
 Peruzzi na Mimi

Jan 1, 2019

TAGOANE LOAN Fund yazinduliwa na Mh. Juliana Shoza


Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza  akitoa wito kwa wasanii wote nchini kujiunga na Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) unaoratibiwa na Taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) leo Jijini Arusha, alipokuwa akizindua mfuko huo ambapo amesisitiza kuwa  wasanii wa makundi yote wanaweza  kujiunga wakikidhi masharti ya kujiunga.


Naibu  Waziri  Mhe.Juliana Shonza ametoa wito kwa  wasanii kujitokeza na kujiunga na Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE LOAN FUND, leo Jijini Arusha  alipokuwa akizindua Mfuko Mkopo wa TAGOANE  LOAN  FUND katika Tamasha la Tukuza Festival  lililoandaliwa na Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE).

Walio vaa scafu za Scout Tanzania ni Kushoto kwa Mh. Juliana Shoza ni Mwanasheria wa TAGOANE Dr. Laltaika, anayefuata Dr. Godwin Maimu Raisi wa Tagoane na Kulia kwae ni Ndugu Silvanus Mumba KAtibu Mkuu Mwenza.

 “Tumekuwa tukishuhudia wasanii wengi wenye majina makubwa wakikosa fedha hata za matibabu  hili limekuwa ni suala lisilo pendeza hivyo ni vyema wasanii mkajiunga katika mfuko huu ambao utawasadia kupata mikopo yenye riba nafau na bima ya afya kupitia hili mnaweza kujikwamua kiuchumi  na kujifunza kuwekeza kwa maisha ya baadae ,“alisema Mhe.Shonza.

Kwa Upande wa Rais wa TAGOANE  Dkt.Godfrey Maimu alifafanua kwamba mfuko huo haubagui msanii kwani  msanii yeyote anayetaka kujiunga anaruhusiwa  kwani lengo la mfuko huo ni kuimarisha umoja wa wasanii na kuhakikisha maisha ya msanii yanaenda kubadilika badala ya msanii kuonekana ni mtu tegemezi  na wakuomba kusaidiwa hata kwenda studio kurekodi.

“TAGOANE tumekuwa tukifanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kusaka vipaji vya uimbaji kwa watoto yatima ambapo lengo ni kuwasadia katika kukuza vipaji vyao lakini  pia na kuwasimamia masuala ya shule katika kuhakikisha  wanapata mahitaji yote muhimu ya shule,”alisema Dkt.Maimu.
Kwa upande wa Katibu Mwenza wa TAGOANE Bw.Silvanus Mumba alieleza kuwa Tamasha hilo kwa mwaka huu limemeendesha Semina ya siku mbili kwa wasanii kuhusu masuala ya Sheria,Sanaa na Ubunifu lengo likiwa ni kumjenga msanii kuendesha shughui zake kwa weledi.


Halikadhalika nae Mmoja wa watoto yatima kutoka Wilaya ya Siha ambaye ni yatima mwenye kipaji cha kuimba nyimbo za injili Witness Justine aliushukuru uongozi wa TAGOANE kwa kumuahidi kumpeleka studio kurekodi nyimbo zake pamoja na kuzitangaza nyimbo hizo pia aliwashukuru kwa kuibua Kipaji chake

Peruzzi na Mimi.