Aug 2, 2012

PERUZZI NA MIMI INAIOMBA SELIKALI IKAE NA WAALIMU KUJADILI JINSI YA KUTATUA MADAI YA WAALIMU


Sheria nayo inatuchanganya, kwasababu ya kuufanya Mgomo wa walimu kuwa batili kwa kipengele cha masaa 24 kuwa ndani ya weekend. Kama ni weekend je inamaana Selikali haiwezi kushughulikia madai ya waalimu kwasababu madai yao yameanzia Weekend?
Tunakoelekea ni walimu kufundisha hata uongo darasani hasa madara ya shule za msingi. hii inasababishwa na madai yao kuwa ni ya msingi, Kiwango cha gharama ya maisha kwasasa kimepanda juu sana lakini mshahara wa waalimu hawa umebaki palepale, wanamudu vipi maisha magumu kiasi hiki?
Selikali imeshindwa kutambua umuhimu wa Waalimu hawa, kwamba bila waalimu maana yake Hatuna waalimu wengine kwa faida ya kizazi kingine, hatuna wachumi, hatuna Malactural, hatuna wanasheria, hatuna washauri wa kibiashara, na kadhalika?
Kwanini Selikali inaingia katika kabishano na Waalimu wakati hata wao wanafahamu fika kuwa Maisha sasa ni magumu wanaishije? 
Je waache kazi wakauze karanga mtaani?
Waache kazi wakafunguwe miradi ya maduka?
waache kazi wakalime?
waache kazi waignie kwenye siasa?
Waache kazi wakapige debe

Na wakiacha kazi nani atafundisha shule zetu ambazo pamoja na uwepo wao kunaupungufu mkubwa sana wa waalimu?
Sel;ikali imewahi kujiuliza kwanini watu wengi sana wanaichukia fani hii ya ualimu? na imechukua hatua gani mpaka sasa tukea mwaka 61 tunapata uhuru?

Kwa mfano; Mwl akimfundisha mtoto wa darasa la I hesabu za kujumlisha kwa kuandika;

1) 1 + 4 = 14
2) 4 x 4 = 44
3) 45 - 5 = 4
4) 45 gawia 5 = 4

Je nani ataenda darasani kukanusha uongo huu au si ndiyo unaweza kuwa mwisho wa kizazi cha somo la Hisabati.

PERUZZINAMIMI inaiomba selikali ikae chini ione huruma kwa Watanzania wenye kipato cha chini, ambao watoto wao wanasoma kwenye shule hizi za Tanzania (kwani Mawaziri watoto zao wako nje, kwahiyo hawata athilika na Mgomo huu Baridi utakao endelea baada uya kuwalazimisha waalimu kwenda makazini bila kutatua matatizo yao)
Silvanus

No comments: