Jan 2, 2013

Ushauri kwa Wasanii wa Filamu (Wanafilamu) Tanzania


Ushauri kwa Wasanii wa Filamu (Wanafilamu) Tanzania

Kutokana na kutokea kwa kifo cha Msanii nguli wa Filamu Tanzania Juma Kilowoko almahalufu SAJUKI, 
Nina machache sana ya kuzungumza na Wasanii, Wadau na Waandaaji wa filamu Tanzania.
Sajuki ni msanii ambaye alikuwa na nia ya kufika mbali na kazi zake zote alizo cheza zilikuwa na mafundisho makubwa mno. Sajuki alikuwa na Mapenzi ya kweli nay a dhati kwa mkewe na wasanii wengine. Mimi namchukulia Sajuki kama mpiganaji, Muelimishaji na mcheshi. Namuombea Baraka tele Wastara kwa kuondokewa na kipenzi chake Sajuki.
Lakini katika mambo ninayo taka kuongea ni hili la kuzingatia sana Bima ya Afya (Medical Insurance), na Mifuko ya kijamii kwa Wasanii.
Jambo hili ni lamsingi sana kwa wasanii kulitolea Macho. Mimi nashangaa sana Eti kuna Raisi wa Shirikisho la filami Tanzania ambaye hana hata Baraza la Mawaziri wala Kamati Tendaji yenye kuleta Tija katika Tasnia hii ya Filamu Tanzania.
Ningewaona Wenye Busara sana kama kungekuwa na Mipango mikakati ya kila Mwaka katika kuhakikisha kuwa Wasanii ambao wako chini ya Raisi wao SIMON MWAKIFAMBA. wanapata vitu vile vya msingi ikiwemo na Medical Insurance, pamoja na kuhakikisha wanajiunga na mifuko ya kijamii, kama NSSF, LAPF, PSPF, na mingine mingi, ili kujiwekea akiba ya uzeeni au hata litokeapo janga au ugonjwa Kama ulio mkuta Ndugu yetu Sajuki.
Sitakikusema nilikuwa nashubiri litokee jambo au nichukulie msiba wa SAJUKI kama mfano lakini nachukulia kama Fundisho la Kila msanii na Huyo RAISI WA SHIRIKISHO ajaribu kufikiria mbinu za kuwanasua kwenye umasikini wa kimawazo Wasanii anao waongoza.
Wenzetu wana Medical Insurance na nilazima kwa msanii yeyote anayecheza Filamu ama Tamthilia kujiunga na BIMA YA AFYA, iko kwenye sheria ya nchi na hiyo walipropose wenyewe wasanii. Hiyo Moja, mbili Lazima msanii aweanalipa kodi ya kila kazi yake inapo ingia sokoni ili kulinda sells flow na mwisho apate kilicho hakiyake, kwa uhakiki wa mamlaka za mapato.
Mwisho napenda kuwapa pole Wasanii wote, nikiwepo na mimi, kwa msiba mkubwa sana kuondokewa na nduguyetu Sajuki Mpiganaji, ila Tuungane tupiganie haki zetu na Tukumbuke Afya zetu.
Mungu ailaze Roho ya marehemu Pema peponi amen.



With Regards
Silvanus C. Mumba
Volunteers Program Coordinator
0713073280/ 0752014077
KOICA Tanzania Office
Phone: 022 244 2324
Fax:     022 244 2297      





Peruzzi na Mimi.

No comments: