Jun 24, 2011

Filamu ya Zombi Bado kidogo Kuisha Editing

Ile filamu ambayo niliiongelea mwezi mmoja ulio pita kwamba nataka kuiandaa ije kufundisha nini kinafanyika katika matendo ya giza ipo karibu kumalizika maandalizi ya Awali. Filamu hiyo ambayo ime andaliwa na ndugu Silvanus C. Mumba (executive produser) na kuchezwa na wasanii mahili sana akiwemo Shiva, Nyemo mabalwe, na wasanii chipukizi wengi wakiwa katika hali ya kimataifa,

Editing ya filamu hiyo imefanyika Hapa Dar es salaam na Mtaalamu kutoka nchini ufaransa kwa jina Awax, na ni professional wa kufanya filamu za aina hiyo, Director wa filamu hiyo ni ndugu Silvanus Mumba ambaye alicheza kama Main character akisaidiana na Awax ambaye alikuwa Camera man.

Naomba ndugu wadau wa filamu mukae mkao wa kula kuisubiria Filamu hiyo iliyo sheheni mafundisho ya kutosha na intertainments, refreshments, comedy, na mengineyo