Jun 1, 2011

Filamu ya Zombie Peak ya Holywood

Nyemo Mabalwe
Huyu ni NYEMORITHA MABALWE
Katika Filamu hii ya ZOMBI amefanya makamuzi ya kufa mtu, na alikutana na magumu mengi sana lakini aliyashinda Challangez hizo ni pamoja na Kuumia, na alisimama yeye kama make up Designer wa Wasanii akishirikiana na KAKA YAKE SILVANUS MUMBA, ambao kwa ujumla ndiyo ma main characters wa filamu hiyo.  Nyemo amecheza kama RITHA Mke wa Russo (SILVANUS) ambaye ni kaka yake wa Damu kabisa lakini kwenye Movie hii ya kutisha na kusisimua waliweka ukaka na udana Pembeni na kufanya makamuzi ya kufa mtu.

Huyu ni Silvanus Mumba
KAKA WA NYEMO. Kijana Silvanus amesimama kama ZOMBI make up designer na ambecheza kama main character katika filamu hiyo ya kusisimua. Silvanus anasema kwa makamuzi aliyo yafanya katika filamu hiyo hana budi kuwaambia Watanzania wote wakae makao wa kula Kusubiri msisimko na Uhondo ulioko katika filamu hiyo ya Kizombie.
Silvanus amejigamba kuwa hata stori yake imetulia na aliitunga kwa kufuata directives za kimataifa na si kukurupuka katika utunzi wa story na Script. Silvanus ameidirect yeye mwenyewe kwasababu amesema Tanzania hakuna Director ambaye angeweza kuidirect filamu hiyo kwasababu wengi wao hukurupuka kufanya kazi ambazo hawana nature nayo wala background ya kazi na mwisho wa siku wanaishia kuiharibu kazi.

Naomba ndigi watanzania muisubiri kwa hamu FILAMU hiyo itakayo kuja kwa jina la ZOMBI.
Raymond Mtapulo
Kijana Ray amecheza Kama Jose Rafiki yake RUSSO, Raymond amecheza kama rafiki wa karibu sana na Russo na ni best friend wa Familia ya Russo, Makazi aliyo yafanya kwenye filamu hii si ya kusimulika lakini mimi nawasihi Watanzania kuisubiri kwa hamu kubwa sana Movie hii.
Charles Magali anasema Yeye amefanya makamuzi ambayo hajawahi kuyafanya katika Movies zote alizocheza Hapa Tanzania kwahiyo Watanzania wakae mkao wa kula kuisubiria Movie hiyo.
Akiongea na Blog hii, Mzee Magali amesema Huyu Director wa Movie hii anauwezo wa Kimataifa na atafika Mbali kwani amemtabiria kufikia peak ya Hollywood.

No comments: