Dec 8, 2011

Bagamoyo » Tanzania Tourist Board

Kisima cha Maji ya Baraka Huko Bagamoyo,, ni ukumbusho wa Baadhi ya mambo ya kale, kisima hiki kilikuwa kinatumiwa na waislamu wa kale na maji yake hayakuweza kuisha tokea enzi hizo mpaka sasa Tembelea Bagamoyo Kaole utapata uhondo huo

Hapa juu ni Kaburi la Wapendanao utaona maelezo kwenye Bango lililo ambatana na Kaburi hilo, Watu hao walikutwa wamekufa wakiwa wamekumbatiana, inasemekana walikuwa wakisafiri kwa boti ndipo walipokutana na umauti huo

Kaburi la Mtoto Sharifa Kitukuu cha Mtume Muhamad,, Mtoto huyo alikuwa anauwezo mkubwa wa kubashiri mambo na yaka tokea alikuwa akiwa Bikra na siku ya kufakwake watoto watatu pia walifariki dunia, na wao wakazikwa pamoja kuzunguka kaburi lake, Fika Bagamoyo Kaole utaona maajabu mengi zaodi ya haya

Kaburi la Ally Bin Juma, Shekhe wa msikiti ambao unakisima cha maji ya Bataka alizikwa eneo la Karibu na Msikiti huo.

  
Namimi nikajiphotoa ukumbushi fasta

  
Kwa mbali ni Eneo ambalo lina msikiti huo wa kale na karibu na upeo wa macho yako ni Baadhi ya misingi ya majengo ya kale ambayo yalifukiwa na mchanga lakini sasa yameonekana

  
Kaburi la sharifa na sisi tukaona isiwe kesi tujiphotoe kitogo tu

  
Msikiti wa Kale uliopo Bagamoyo huko Makumbusho ya Kaole


Endelea kupata uhondo wa Mabaki ya Kale yaliyoko bagamoyo,, Ni vema kwenda na kujionea mwenyewe kwa macho it is like free Tanzania Shiling 1500 tu entrance









Asante sana Munakaribishwa sana Bagamoyo

Bagamoyo » Tanzania Tourist Board


Silvanus

No comments: