Dec 15, 2011

TAASISI YA USTAWI WA JAMII INATOA TAARIFA KWA UMMA




TAASISI YA USTAWI WA JAMII (lSW) ILIYOKO KIJITONYAMA MJINI DAR ES SALAAM, INAPENDA KUUTAARIFU UMMA WA WATANZANIA KUWA TAYARI IMEFANIKIWA KUKIDHI MAHITAJI NA MATAKWA YALIYOTOLEWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) NA KUPATA ITHIBATI (ACCREDITATION).

KUTOKANA NA HATUA HIYO, MWENYEKITI WA BODI YA MAGAVANA WA TAASISI PROFESA LUCIAN MSAMBICHAKA KWA·NIABA YA BODI YAKE ANA WATAARIFU, WANAFUNZI, WAZAZI, WALEZI NA WATANZANIA KUWA HIVI KARIBUNI ITAANZA KUFANYA UDAHILI KWA AJILI YA WANAFUNZI WA MWAKA.WA KWANZA WANAOTAKA KUCHUKUA MASOMO KWAAJILI YA CHETI, STASHAHADA, SHAHADA YA KWANZA NA STASHADA YA UZAMIVU.

MWENYEKITI WA BODI YA MAGAVANA PIA ANATOA SHUKRANI KWA UONGOZI WAWIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII CHINI YA WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII MHESHIMIWA DK. HAJI HUSSEIN MPONDA (MB), NAIBU WAZIRI MHESHIMIWA DK. LUCY NKYA (MB) NA KATIBU MKUU MHESHIMIWA BLANDINA NYONI KWA KUFANIKISHA MCHAKATO HUO.

SHUKRANI NYINGINE ZIWAFIKIE MGANGA MKUU WA SERIKALI (CMO) DK. DEO MTASIWA, MKURUGENZI WAMAFUNZO DK. GILBERT MLIGA, KAMISHNA WA USTAWI WA JAMII NDUGU DUNFORD MAKALLA.

AIDHA,MWENYEKITI WA BODI ANAISHUKURU KWA DHATI TIMUYA WATAALAM WALIOHUSIKA KUFANYA UHAKIKI WA NYARAKA ZA TAASISI IKIONGOZWA NA PRO. MONGULA, MENEKIMENENTI YA TAASISI NA SERIKALI YA WANAFUNZI KWAKAZI NZURI ILIYOFANIKISHA KUFIKIWA KWA HATUA HII MUHIMU.

AHSANTENI.

'PRO: LUCIAN MSAMBICHAKA
MWENYEKITI
BODI YA MAGA VANA



No comments: